Kundi la watafsiri limo mbioni

 •  Magazeti yata tafsiriwa kwa lugha ya Russia, Kingereza, Kiswahili, Lingala, Kifaransa,  Kichina, Kiarabu na Kipolish (lugha ya Poland).
 • Tafsiri za kwanza zitaonekana hivi karibuni katika blogi za Magazeti ya Häme.
 • Wazo ni kwamba kila mtu aweze kutafsiri mambo mbalimbali ya mhimu yenye kuwa kwenye magazeti.

TUULIA VIITANEN Maandishi// TONI RASINKANGAS Picha

 

Maulizo:

 1. Wewe ni nani?
 2. Kwa nini umekuja Finland?
 3. Umefanya nini maishani mwako na ni ipi kazi yako?
 4. Kwa nini umejiunga kwa kikundi cha watafsiri?
 5. Ni ipi kauli mbiu yako?
 6. Ni lipi neno zuri kwa lugha ya kifini?

 

 1. GHISLAINE CEUSI KYUBWA. Mimi ni Mkongomani, nimeolewa na ni mama wa watoto wa tano. Nimehamia Finland na familia yangu ndogo mwishoni mwa mwaka 2010.
 2. Nimekuja Finland kupitia  mkataba kati ya umoja wa mataifa yenye kuhudumia wakimbizi(UNHCR), serekali ya Rwanda na Finland kwa sababu mimi ni mkimbizi aliyekubaliwa na Finland kabla ya kuhamia huko.
 3. Nimefanya kazi ya mwalimu  inchini Kongo na Rwanda, pia kama mfanyakazi wa jamii katika kambi la wakimbizi inchini Rwanda. Inchini Finland nimefanya kazi kama mwalimu wa lugha ya kiswahili pia kama mkalimani. Kazi yangu rasmi, mimi ni mwalimu ila  hapa Finland nimesoma kama msaidizi wa mwalimu Shuleni.
 4. Nimejiunga kwa kikundi cha watafsiri kwa maana nataka kuboresha ujuzi wangu wa lugha ya kifini ata lugha zingine ambazo nazi fahamu. Ila kitu kikubwa ni kwamba ningependa kusoma kama mfanya kazi wa jamii.
 5. Kauli mbiu yangu ni:” Mimi sirudi nyuma”
 6. Kwangu mimi neno zuri kwa kifini ni ”äidinkieli”(lugha ya mama).

 

 1. PETRA PALJAKKA. Mimi nimeishi mda mrefu wa maisha yangu inchini Ubelgiji na nimesoma shule la sekondari inchini Finland.
 2. Shule la sekondari.
 3. Mimi ni mwanafunzi wa shule la sekondari na nilikuwa kwa mazoezi ya kazi mkoani Vila.
 4. Napenda ku chukuwa fursa ya kuboresha ujuzi wa lugha yangu ya Kifini pia kupata uzoefu katika mambo mbalimbali.
 5. Mtazamo wako unaleta suluhisho (ukitaka utaweza)
 6. Liplattaa( kutoa sauti ya maji wakati wa mawimbi madogo)

 

 1. GUNTA KARAPALO.
 2. Uhusiano wa familia. Mume wangu ame amua kurudi aliko zaliwa, hiyo ikatufanya kurudi familia yote  incnini Finland.
 3. Kazi yangu ni mhandisi wa ujenzi. Nilipo maliza kusoma kwenye Chuo kikuu cha Sayansi ya Kilimo, nime fanya kazi kama mhandisi mda wa myaka sita. Kazi yangu ili badilika hapo nilipo anza kazi ingine katika uwaziri wa uchumi kama msaidizi katika mambo ya kimataifa. Nilifanya kazi huko mda wa myaka tisa. Kiisha nikafanya kazi kama mkurugenzi wa miradi na usafirishaji katika Shirika la maendeleo  mnamo maeneo ya Courland. Nilifanya kazi hiyo mda wa myaka saba. Finland nimefanya kazi kama mfanyakazi wa ofisi katika Shirika la Setlementti  mkoani Hämeenlinna.
 4. Nataka kuboresha  na kujua kifini ili nipate kazi siku za usoni.
 5. Mimi nakubaliana na Martin Luther ambaye alisema:” Ata ninge fahamu dunia inafika mwisho, leo nita panda mti wa apple.”
 6. Avaruus (nafasi ya juu)

 

 1. BOTOND VEREB-DÉ, mwanzilishi wa mradi” Renessanssi” katika  mji wa Hämeenlinna, nimehamia  inchini Finland nikitokea inchi ya Hungary myaka minane iliyo pita.
 2. Finland ime nifanya kupenda  Kifini na kupata kazi. Nimesoma  Kifini  katika chuo kikuu inchini Hungary na hii ika nifanya kuhamia Finland ili nifanye kazi.
 3. Ujuzi wangu wa Kifini uli nifanya kupata  uhalali wa kufanya kazi katika miradi ya huduma kwa wateja. Nimeenza  kazi maeneo ya kaskazini  mwa Finland ya ukalimani na kushurulika na mambo mbalimmali ya wafanyakazi, kiisha hapo nika hamia mkoani Tampere. Hivi sasa nina fanya kazi maeneo ya Hämeenlinna tangu miezi mitatu. Mkoa wa Hämeenlinna unajitahidi kuleta suluhisho iwezekanavyo kwa wasio na kazi ili waweze kusaidiwa kupata angalao kitu cha kufanya. Na hii ndio lengo la mradi huu.
 4. Wazo la mradi huu limeanzishwa ili watakao fanya kazi hiyo ya utafsiri waweze angalao kupata maneno mapya na kuboreha sarufi katika lugha ya Kifini. Washiriki watafanya kazi ngumu na nina amini ujuzi wao wa lugha utaendelea vizuri mda huu wa mradi. Vivyo hivyo wakaaji wa Hämeenlinna wanaweza kusoma magazeti kwa lugha za kigeni wanazo zielewa na kupata habari mbalimbali.
 5. Kauli mbiu yangu ni ” Fikiri kwa ujumla na utende ki pekee”
 6. Vauva (mtoto) Lakini zaidi ya hii napenda neno Musiikki (muziki) kwa sababu kuna kama melodia katika lugha ya Kifini.

 

 1. JING YU-HELLBERG. Nimetoka inchi ya Uchina.
 2. Naishi Finland kwa mda wa myaka  mitano. Mume wangu ni Mfini. Baba yangu na dada zangu wanaishi pia Finland ndio maana nime amua kuhamia Finland.
 3. Nime fanya, katika inchi ya Uchina, kazi ya mda mfupi katika sekta ya kubuni( kupangilia) graphic.
 4. Nimependelea kujiunga kwenye kundi la watafsiri kwa sababu lita nisaidia kujifunza vizuri kifini.
 5. Kauli mbiu yangu ni ” Kesho ni siku mpya.”
 6. Neno zuri kwa lugha ya Kifini ni kiitos ( asante/aksanti)

 

 1. NAURIS ”NAKKE” AVOTS, nimetokea inchi ya Latvia na mimi ni mhimizaji/kiongozi wa kikundi hiki.
 2. Nilikuja Finland kwa ajili ya asili na lugha ya Finland, pia kupitia rafiki yangu mfini aliye nisaidia.
 3. Nimefanya kazi mbalimbali ila kubwa katika hizo ni kazi za kufundisha kifini, kutafsiri na ukalimani.
 4. Ningependa washiriki wangu wa kikundi cha watafsiri wapate wito wa kazi hii ambao ina julikana kuwa mpya kwao. Nita jitahidi kutoa mafunzo yalio ya kipekee kwa washiriki wangu.
 5. Kauli mbiu yangu ni ”Tulianzalo mapema na tulimalize mapema”
 6. Nauris ( jina la mboga za majani)

 

 1. NADEZDA” NADIA” UIDINA
 2. Upendo. Mwaka wa 2007 nimeolewa na mume anayeishi inchini Finland.
 3. Nimefanya kazi  mbalimbali inchini  Russia na Finland: inchini Russia nime fanya katika maabara ya picha.  kazi yangu maarufu ilikuwa  ku chunguza na ku hariri picha. Inchini Finland nilifanya kazi ya usafi, seremala na katika sekta ya vifaa kama meneja wa ghala( logistic). Kazi yagu rasmi ni seremala na meneja wa ghala.
 4. Kitu kikubwa nataka kuendelea mbele katika lugha ya kifini. Naamini nita pata kazi mpya, ambayo haita nifanya nifanye kazi usiku, kwa sababu nataka kupata mda wa kutosha wa kuwa na mwanangu.
 5. Fikiri vyema, sabatamu kila wakati, mambo mazuri yako mbele.
 6. Unelma( ndoto)

 

 1. MUSTAFA KARIM ABDULLAH. Mimi ni mkimbizi toka inchi ya Iraq.
 2. Nimekuja tarehe 13.8.2013, kwa sababu sikuweza kuishi katika inchi ya Iraq.  Kulikuweko na rushwa katika kampuni ya umeme na mimi nili taka ku zuia hiyo, ndipo wapiganaji wa chama fulani wali jaribu kuniua. Hiyo ikanifanya nitoke Iraq.
 3. Nimesoma inchini Iraq kwenye chuo kikuu cha uhandisi wa umeme. Finland nime soma kifini.
 4. Nataka kuboresha ujuzi wa lugha ya kifini hivi nipate kufanya kazi ao kusoma kiwango cha juu cha uhandisi wa umeme.
 5. Jaribu kuishi kwa thamani na amani.
 6. Mukava(vizuri)

 

 1.  MOZART MAMBONGA. Nimetokea inchini Kongo.
 2. Vita  vya wenyewe kwa wenyewe inchini Kongo.
 3. Nina fanya kazi kwa sasa kwa shirika la  Setlementti lipatikanalo kwa Kumppanuustalo.
 4. Napenda kuwasaidia wakongomani kuelewa kifini na zaidi ya hayo nataka kutumia lugha yangu ya mama. Ninge penda  ku tengeneza kamusi ndogo ya Lingala.
 5. Uwe mjasiri.
 6. Mwenye furaha.

 

 1. PIOTR KASPEREK. Mimi ni mwanamume mpolandi wa myaka 21.
 2. Nimekuja Finland kwa  sababu ya wazazi wangu. Myaka tano iliyo pita baba yangu  ali hamia Finland kwa sababu ya kikazi na myaka mitatu baadae mama yangu ali amua kuja kuishi na mume wake. Hapo ndipo na mimi nili amua kuhama pamoja nao.
 3. Mimi sina kazi kwa sasa. Nilipo maliza shule la sekondari nili hamia hapo hapo Finland. Kwa sababu za uhamiaji siku weza kupata kazi inchini Poland.  Maisha yangu ya kikazi imeanzia Finland, niliko fanya mazoezi mbalimbali ya kazi.
 4. Napendelea kikundi hiki cha watafsiri kwa sababu naamini itanisaidia kuboresha ujuzi wangu wa  kifini na kuni tayarisha ipasavyo  kwa kazi ya utafsiri, hiyo ambayo naipenda sana, inchini Finland.
 5. Kila watu walitakalo hawajali umbali wa huko waendapo kwa sababu hakuna yeyote atakae waletea msaada ila  wao wenyewe.
 6. Kifini ni lugha  nzuri, ndio maana ni jambo ngumu kuchagua neno moja peke yake. Lakini mimi nachagua neno” Matka”. Neno hili lina maanisha katika lugha yangu ”mama”

Kommentointi on suljettu.

css.php